Biashara ya Ubadilishaji Fedha za Kigeni Mpakani Tunduma Yawaibua BOT Kwenda Kutoa Elimu
Автор: StudioNative
Загружено: 2023-12-23
Просмотров: 307
Описание:
Changamoto katika biashara ya kubadilisha fedha za kigeni hususani katika maeneo ya mipakani imepewa mwarobaini kwa Benki Kuu Tanzania (BOT) kuwapunguzia gharama wafanyabiashara ambao wanaomba leseni za kufungua maduka ya kubadilisha fedha za kigeni pamoja na kuwapunguzia viwango vya mitaji kwa kila daraja ambalo mfanyabiashara anamudu.
Hayo yamebainishwa na Amri Mbalilaki ,Mkuu wa kitengo cha uchunguzi BoT katika kikao cha BOT pamoja na wadau wa masuala ya fedha hususani wafanyabiashara wa fedha za kigeni katika kikao kilichofanyika Tunduma ambapo kuna muingiliano mkubwa wa fedha za kigeni.
CUE…………………. AMRI MBALILAKI (MKUU WA KITENGO CHA UCHUNGUZI BOT)
Akizungumza katika kikao hicho Afisa Kurugenzi ya Usimamizi wa sekta ya Fedha kutoka benki kuu amewataka wadau hao kufanya biashara hiyo na wafanyabiashara waliorasimishwa ili kuepukana na uhujumu uchumi na kuona pato la taifa likiongezeka.
CUE………………. ABDUL MUSSA
Kwa upande wao wafanyabiashara hao wameipongeza BOT kwa kutoa elimu na kuendesha semina hiyo yenye faida kwao lakini wakiomba serikali kuwa na sera moja pasipo kubadilisha sera kila wakati ili wafanyabiashara hao wafanye biashara kwa uhuru huku elimu zaidi ikisisitizwa kuendelea kutolewa.
CUE…………………. HERRY SANGA MFANYABIASHARA TUNDUMA
CUE………………….. ELIJAH SIMBEYE MFANYABIASHARA TUNDUMA
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: