DC MWAIPAYA AHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA, KUGOMBEA NA KUPIGA KURA
Автор: KUSINI YETU ONLINETV
Загружено: 2024-10-05
Просмотров: 110
Описание:
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, mkoani hapa, Mhe. Abdallah Mwaipaya ametoa wito kwa wakaazi wa wilaya hiyo kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, kujitokeza kugombea nafasi za uongozi na kushiriki kwenye zoezi la kupiga kura ili kutimiza haki yao ya msingi ya kikatiba, katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu.
Mwaipaya ametoa wito huo leo Oktoba 5, 2024, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, ambapo amesema pamoja na masuala mengi muhimu, lakini anawasisitiza wananchi kuwa mstari wa mbele kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura ambalo litaanza kufanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 20, mwaka huu.
Aidha amevitaka vyama vyote vya siasa kujitokeza kugombea nafasi hizo za uongozi pamoja na kuhamasisha wanachama wa vyao kushiriki uchaguzi huo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: