USHIRIKIANO WA TANZANIA NA MAREKANI KUKUZA MIGODI KUSINI
Автор: JUHUDI DIGITAL
Загружено: 2026-01-21
Просмотров: 48
Описание:
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Madini na Nishati ya Marekani inaandaa utekelezaji wa mradi mkubwa wa utafiti wa kina wa madini, unaolenga kuimarisha agenda ya maendeleo ya sekta ya madini nchini.
Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma, Mhe. Mavunde amesema ushirikiano huo unalenga kuimarisha mahusiano ya kimkakati kati ya Tanzania na Marekani, pamoja na kujenga uwezo wa kitaalamu kwa Watanzania wanaofanya kazi katika sekta ya madini, hususan katika eneo la utafiti wa kina wa rasilimali za madini.
Amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za madini ya aina mbalimbali, hali ambayo imeifanya nchi kuwa na nafasi muhimu katika kukidhi mahitaji ya madini yanayoongezeka duniani.
Kwa mujibu wa Waziri Mavunde, yapo maeneo yenye leseni za madini yanayomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ambapo kupitia ushirikiano huo, Tanzania na Marekani zitafanya utafiti wa pamoja ili kubaini maeneo yenye fursa kubwa za uwekezaji wa kimadini.
“Utafiti huu wa pamoja utatusaidia kubaini maeneo yenye utajiri mkubwa wa madini na kufungua fursa za uwekezaji, jambo litakalosaidia kuanzishwa kwa migodi mikubwa mipya, hususan katika mikoa ya Mtwara na Lindi,” amesema Mhe.Mavunde
Ameongeza kuwa Serikali ya Marekani imeonesha utayari wa kushirikiana na Tanzania katika kupanua maeneo ya utafiti wa madini pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Kitanzania, ili kuwawezesha kusimamia ipasavyo rasilimali za madini kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Waziri Mavunde amesema eneo linalotarajiwa kufanyiwa utafiti wa kina lina madini muhimu yanayojulikana kama madini kingwe (graphite), ambayo mahitaji yake duniani yanatarajiwa kufikia tani milioni 4.5 kwa mwaka ifikapo mwaka 2050.
“Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kuwa miongoni mwa wasambazaji wakubwa wa madini ya graphite duniani kutokana na rasilimali tulizonazo,” amesema.
#wizarayamadini
#habari
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: