Video: Mbunge jimbo la Segerea, afunguka baada ya kulalamikiwa kuhusu mfuko wa jimbo
Автор: Nasahaplustv
Загружено: 2017-08-03
Просмотров: 1852
Описание:
Mbunge Jimbo la Segerea amefunguka na kushauri serikali ifanye utaratibu wa kuwapa semina madiwani wa baraza la madiwani Halmashauri ya wilaya ya Ilala kuhusu matumizi ya mfuko wa jimbo maana wengi wamekuwa hawana elimu kuhusu suala hilo.
Hatua ya Mbunge huyo kufunguka imekuja baada ya Diwani wa Kata ya Kipawa Saimoni Kenedy kudaikutoshirikishwa na mbunge huyo katika masuala ya mfuko wa jimbo jambo ambalo mbnge huyo amelikanusha vikali.
Mbunge Bonnah ameeleza kuwa kunabaadhi ya madiwani wanaamini mfuko wa jimbo pesa zinakaa nyumbani kwake jambo ambalo siyo kweli, mfuko wa jimbo una kamati zake na pesa hizo zinakaa serikalini mpaka itokee changamoto ndiyo zinaombwa kwaajil ya utatuzi.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko amemuagiza Kaimu Mchumi Mussa Liute kuitisha kikao kitakachomshirikisha mbunge na madiwani ili kujadili na kuona jinsi mfuko wa jimbo ulivyotumika katika jimbo hilo na kumpelekea ripoti.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: