NIRC YAAHIDI MAJI YA UHAKIKA KWA UMWAGILIAJI JOBAJI
Автор: Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC)
Загружено: 2025-12-21
Просмотров: 20
Описание:
📍NIRC Karatu, Arusha.
Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imewaasa wakulima wa skimu ya Umwagiliaji Jobaji iliyopo wilayani Karatu Mkoani Arusha kuwa wastahamilivu, katika kipindi ambacho Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika Skimu hiyo.
Tume imesema ni wajibu wa serikali kuhakikisha wakulima wanapata maji ya kutosha ili kuwa na kilimo cha uhakika.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uendeshaji Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Salome Njau, wakati wa mafunzo ya Uendeshaji, Usimamizi na Matunzo ya skimu ikiwa ni utekelezaji Mradi wa Mifumo Himilivu ya Chakula nchini (TFSRP-P4R).
Amesema ni wajibu wa Serikali kuhakikisha mkulima anakuwa na uhakika wa Kilimo kwa kupata maji ya kutosha kumwagilia mazao.
Amesema licha Serikali kuendelea na ujenzi wa bwawa katika bonde la Eyasi, pia inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji, ili kuhakikisha inadhibiti upotevu wa maji, unaochangiwa na ubovu wa miundombinu pamoja na miundombinu ya asili, ambayo haijasakafiwa na kujengwa kitaalamu.
Amekiri kuwa changamoto inayowakabili wakulima wa skimu hiyo, kwa sasa ni ukosefu wa maji ya kutosha kufika mashambani kutokana na kutokuwa na miundombinu madhubuti inayopusha upotevu wa maji.
Amesema kwa kuwa Serikali inahakikisha wakulima wanapata maji ya kutosha mashambani, Tume inaendelea uchimbaji wa visima, vyenye uwezo wa kuchimba visima vyenye urefu zaidi mita 1000, hivyo itahakikisha kuwa mkulima anapata maji kwa uhakika.
Hata hivyo baadhi ya wakulima walioshiriki mafunzo ya Usimamizi, Uendeshaji na Matunzo ya skimu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya mgawanyo wa maji kutokana na kutokuwa na bwawa la kuvuna maji, pamoja na mifereji hafifu inayosababisha upotevu wa maji.
Wakulima hao Wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mafunzo hayo, kwani awali walikuwa wanafanya shughuli za kilimo kienyeji na kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuilinda miundombinu dhidi ya uharibifu na itadumu kwa muda mrefu.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Tufuatilie kupitia mitadao yetu ya kijamii
Instagram: https://www.instagram.com/nirc_tz?igs...
Facebook: / tumeyaumwagi. .
XTwitter: https://x.com/nirc_tz?t=UoFluCQyTUnM4...
LinkeInn: / tume-ya-taifa-ya-umwagiliaji-national-irri...
_______________________________________________________________________
#01trending #tanzania #umwagiliaji #kilimo #kilimobiashara #kilimochaumwagiliaji #MAKALA #story #storybook #ikulumawasiliano #DktSamiaSuluhuHassan #Rais #agriculture #agranews #agranewstoday #agricultural #agronomia #agroecologie #agriculturelife #agriculturalmachinery #kilimoufugaji #agrieconomy #kilimo #trendingtanzania #ikuluzanzibar #ikulutanzania #ikulu #ccm #ccmtz #chamachamapinduzi #agrfilms #agrf2023 #cnbctv #cnbcnews #kbcchannel1
National Irrigation Commission
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: