📌Wanawake Waitwa Kutatuliwa Kero Za Ardhi.
Автор: TANZANIA YETU HABARI
Загружено: 2026-03-01
Просмотров: 134
Описание:
Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Kilimanjaro,Rehema Mdee, Ametoa wito kwa Wanawake Mkoani Humo Kujitokeza Kuanzia March 2-07,2026 Kupata elimu Sambamba na Kupata Utatuzi wa Kesi zinazohusu Ardhi zonazowakabili.
Amesema Hayo Wakati akizungumza na Wanahabari Kuelekeza Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa machi nane ya kila mwaka.
Amesema Sera ya Ardhi Imetambua kuwa Mwanamke kama alivyo Mwanaume anahaki ya kumiliki Ardhi Hivyo wamejipanga Kutoa elimu Hiyo kwa Wanawake ili kuondoa dhana potofu ya wanawake kumiliki Ardhi.
Aidha Ameeleza kuwa Kliniki hiyo kwa Jina la Samia Ardhi Kiliniki Inayofanyika katika mikoa na halmashauri zote nchini itatoa huduma kwa Wanawake wote wenye shida za ardhi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Kliniki hiyo imebebwa na Kauli Mbiu “Mwanamke; Haki Yako, Miliki Sasa,” ikilenga kuwafikia wanawake wengi zaidi na kuwawezesha kumiliki ardhi, Wakati huu ambao ni asilimia 28 tu ya wanawake wanaomiliki ardhi nchini.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: