ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

Jionee Ziara ya Waziri wa Ulinzi na JKT Alipotembelea Kamandi ya NAVY

Автор: Ulinzi Channel

Загружено: 2021-10-14

Просмотров: 123960

Описание: Tarehe 12 Oktoba, 2021 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax (Mb) amefanya ziara ya kutembelea Kamandi ya Jeshi la Wanamaji (Navy Command) iliyopo eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri ametembelea Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kutembelea Kamandi za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania MKOANI Dar es Salaam, kwa lengo la kujitambulisha, kujionea utayari kiutendaji, miundo pamoja na changamoto na namna wanavyokabiliana nazo kiutendaji katika kulinda mipaka ya nchi yetu kwa upande wa baharini na kwenye maziwa.
Alipowasili Makao Makuu ya Kamandi hiyo alipokelewa na mwenyeji wake amabye pia, ni Mkuu wa Kamandi hiyo, Meja Jenerali Michael Mwanandenje Mumanga akiwa pamoja na wanadhimu wa Kamandi, Wakuu wa Vikosi na Shule pamoja na maafisa.
Mara tu baada ya kuwasili Makao Makuu ya Kamandi, Mheshimiwa Waziri alipokea Salaam ya Heshima iliyoandaliwa na Gadi ya Mapokezi na kisha kusaini Kitabu cha Wageni, kabla ya kutembelea gati (dockyard) na chelezo (slipway) na ujenzi wa Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto unaotekelezwa na Kamandi hiyo kwa kutumia fedha za ndani. Jengo hilo litapokamilika litakuwa limegharimu takribani milioni 120 na pia, litatoa huduma za matibabu kwa familia za Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma pamoja na wananchi waishio maeneo ya jirani.
Baada ya Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax kupatiwa Taarifa ya Utendaji ya Kamandi ya Jeshi la Wanamaji, iliyosomwa kwake na Meja Jenerali Mmanga, Taarifa iliyohusu Historia, Mkao wa Kamandi, Majukumu ya Kamandi, Maeneo ya Uwajibikaji, , Changamoto ya Miundombinu Zana na Vifaa, Mkakati wa Kamandi pamoja na Mapendekezo ya Kamandi ya kukabiliana na changamoto ziliyowasilishwa kwake.
Akitoa taarifa ya Kamandi Jenerali Mmanga alimweleza Mhe Waziri kuwa, Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ikiwa ni sehemu ya JWTZ, yenye majukumu makuu mawili. Majukumu hayo ni yale ya kiasili (Traditional Roles) yanayojumuisha kuimarisha ulinzi wa mipaka ya baharini na kwenye maziwa, operesheni zote ndani na nje, kusindikizaa meli za Biashara za hapa nchini na za nchi rafiki, kutoa misaada ya utaftuataji, uokoaji na uopoaji wa watu na vifaa kutoa misaada wakati wa maafa na majanga kwa kushirikiana na vikundi vingine, kufanya shughuli za kidiplomasia kwa meli zetu kutembelea mataifa mengine pamoja na kulinda raslimali za nchi yetu zinazopatikana baharini.
Aidha, Meja Jenerali Mumanga alibaianisha aina ya pili kuwa ni yale majukumu ya kupambano dhidi ya uhalifu baharini na kwenye maziwa (Contemporary maritime Roles) yanayojumuisha utekaji na uporaji, ugaidi baharini, biashara za magendo, uvuvi haramu uchafuzi wa bahari, usafirishaji na usambazaji wa madawa ya kulevya pamoja na uhamiaji haramu.
Mara tu baada ya kupewa taarifa hiyo, Dkt. Stergomena Lawrence Tax alimshukuru Mkuu wa Kamandi na Maafisa Wanadhimu kwa mapokezi mazuri aliyoyapata baada ya kuwasili hapo Makao Makuu ya Kamandi pamoja na taarifa nzuri iliyompa mwanga katika kutekeleza majukumu yake ndani ya Wizara.
Aidha, Mheshimiwa Waziri aliweka bayana kuhusu madhumuni ya ziara yake kwenye Kamandi hiyo, kuwa ililenga kuwatembelea kwa lengo la kujitambulisha, kufahamiana, kujifunza shughuli mbalimbali wanazozifanya pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo. Na kupitia mhadhara huo, ameweza kujifunza mengi.
Kuhusu changamoto, Mheshimiwa Stergomena Lawrence Tax amewaasa Wanamaji kuwa changamoto ni nyingi na ni halisi, cha msingi ni kuzifanyia uchambuzi wa kina kuona ni zipi ziweze kuchukuliwa hatua na Wizara kwa kuzingatia vipaumbele na zile changamoto ndogondogo ambazo ziko ndani ya uwezo wao waendelee kuzifanyia kazi.
Mwisho Mheshimiwa Waziri aliwataka kuendelea kutekekeleza majukumu yao kwa weledi, maana Jeshi ni watu wanaofanya kazi kwa weledi.

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
Jionee Ziara ya Waziri wa Ulinzi na JKT Alipotembelea Kamandi ya NAVY

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

WAZIRI WA ULINZI NA JKT DKT. STERGOMENA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA KAMANDI YA JESHI LA AKIBA MANYONI

WAZIRI WA ULINZI NA JKT DKT. STERGOMENA ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA KAMANDI YA JESHI LA AKIBA MANYONI

Военные массово пошли против Кремля / Срочное обращение к властям

Военные массово пошли против Кремля / Срочное обращение к властям

Открытие Варбурга: 4 переключателя, которые мешают раку расти | Здоровье с Доктором

Открытие Варбурга: 4 переключателя, которые мешают раку расти | Здоровье с Доктором

EXTENDED HIGHLIGHTS | DAKIKA 30 ZA BURUDANI | KMC FC (0) VS SIMBA SC (2) | LIGI KUU YA NBC 2025/26

EXTENDED HIGHLIGHTS | DAKIKA 30 ZA BURUDANI | KMC FC (0) VS SIMBA SC (2) | LIGI KUU YA NBC 2025/26

MBWEMBWE ZA WANAJESHI JWTZ NA CHINA, SILAHA NZITO, NYIMBO ZAO

MBWEMBWE ZA WANAJESHI JWTZ NA CHINA, SILAHA NZITO, NYIMBO ZAO

⚠️ NETANYAHU AFANYA UMAFIA MZITO KWENYE IKULU YA MAREKANI! MBELE YA RAIS TRUMP

⚠️ NETANYAHU AFANYA UMAFIA MZITO KWENYE IKULU YA MAREKANI! MBELE YA RAIS TRUMP

AMKA NA BBC SWAHILI ASUBUI HII LEO ALHAMISI

AMKA NA BBC SWAHILI ASUBUI HII LEO ALHAMISI

WAZIRI WA ULINZI NA JKT ATEMBELEA KAMANDI YA JESHI LA ANGA

WAZIRI WA ULINZI NA JKT ATEMBELEA KAMANDI YA JESHI LA ANGA

TAZAMA MAKOMANDO WA JWTZ WALIVYOTANDA KWENYE MELI YA KIVITA ILIYOMBEBA MKUU WA MAJESHI, ULINZI MKALI

TAZAMA MAKOMANDO WA JWTZ WALIVYOTANDA KWENYE MELI YA KIVITA ILIYOMBEBA MKUU WA MAJESHI, ULINZI MKALI

😱 KHAMENEI AOMBA RADHI!

😱 KHAMENEI AOMBA RADHI! "YALIYOPITA SI NDWELE" - MAZITO KUHUSU MAANDAMANO IRAN YAMEFUNULIWA

UTAPENDA, Waziri wa Ulinzi na Jkt, Mhe. Dkt Tax Ashuhudia Maonyesho ya Ndege za Mafunzo Tanga

UTAPENDA, Waziri wa Ulinzi na Jkt, Mhe. Dkt Tax Ashuhudia Maonyesho ya Ndege za Mafunzo Tanga

Waziri Stergomena Tax Afurahishwa na GUARD YA MAPOKEZI ya Wanajeshi Wanawake  DFHQ

Waziri Stergomena Tax Afurahishwa na GUARD YA MAPOKEZI ya Wanajeshi Wanawake DFHQ

MIAKA 60 YA UHURU, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Aelezea Mafanikio.

MIAKA 60 YA UHURU, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Aelezea Mafanikio.

Дудаев об Украине, Советском Обмане и Имперской Лжи: Что Джохар написал об этом за день до смерти.

Дудаев об Украине, Советском Обмане и Имперской Лжи: Что Джохар написал об этом за день до смерти.

Ziara ya Waziri wa Ulinzi na JKT Alipotembelea Makao Makuu ya JKT

Ziara ya Waziri wa Ulinzi na JKT Alipotembelea Makao Makuu ya JKT

WAZIRI BASHUNGWA AKIMWAGIA SIFA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI -NDC AONGEA NA MAAFISA NA ASKARI

WAZIRI BASHUNGWA AKIMWAGIA SIFA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI -NDC AONGEA NA MAAFISA NA ASKARI

Kwata la kimyakimya la Wanajeshi wa Tanzania Uhuru Day 2016

Kwata la kimyakimya la Wanajeshi wa Tanzania Uhuru Day 2016

Rais Kikwete  alipowatunuku Kamisheni maafisa 437 wa Jeshi la Kongo na JWTZ Monduli Arusha

Rais Kikwete alipowatunuku Kamisheni maafisa 437 wa Jeshi la Kongo na JWTZ Monduli Arusha

Почки скажут вам: всего 1 стакан перед сном и ночные походы в туалет исчезнут | ПАМЯТЬ И МОЗГ

Почки скажут вам: всего 1 стакан перед сном и ночные походы в туалет исчезнут | ПАМЯТЬ И МОЗГ

LIVE: MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI (ABC 2026) - SIKU YA KWANZA, DODOMA

LIVE: MKUTANO MKUU WA MWAKA WA VYOMBO VYA UTANGAZAJI (ABC 2026) - SIKU YA KWANZA, DODOMA

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]