SIKU YA MTINDIO WA UBONGO
Автор: CLOUDS HABARI
Загружено: 2025-10-06
Просмотров: 42
Описание:
SIKU YA MTINDIO WA UBONGO
Kila mwaka tarehe 6 Oktoba, dunia nzima inaadhimisha siku ya mtindio wa ubongo, ikiwa ni katika harakati za kuhamasisha, kuelimisha na kuchukua hatua ili kuhakikisha watu wenye tatizo la mtindio wa ubongo, wanapata haki ya kufikiwa na fursa mbalimbali sawa na mtu mwingine yeyote katika jamii zao.
Ugonjwa wa mtindio wa ubongo unaoathiri ukuaji wa mwili umemulikwa hii leo ambayo ni siku ya kuhamasisha dunia juu ya ugonjwa huo ambao umeenea maeneo yote duniani.
Shirika la afya duniani, WHO linaeleza kuwa ugonjwa huo hujitokeza mwanzoni kabisa mwa uhai wa mwanadamu na chanzo ni hitilafu za mishipa ya fahamu ambayo hatimaye huathiri utendaji wa ubongo.
Maadhimisho hayo ni hatua mojawapo ya kuhakikisha kwamba watu wenye matatizo hayo wanatendewa haki.
Hali hiyo inaweza kumfanya mtu kukosa mawasiliano ya moja kwa moja baina ya viungo vyake na akili.
Kwanza tuangalie Utindio wa ubongo ni nini…. Wataalamu wanasema kuwa mtindio wa ubongo ni kundi la matatizo yanayoathiri uwezo wa mtu kutembea na kudumisha usawa na mkao sahihi.
Tatizo hili husababishwa na maendeleo yasiyo ya kawaida ya ubongo au uharibifu katika ubongo unaokua, ambao huathiri uwezo wa mtu kudhibiti misuli yake.
Ni hali maarufu zaidi ya ulemavu wa mwendo (movement disability) kwa watoto.
Hali hii hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine ambapo mtu mwenye utindio wa ubongo kwa kiasi kikubwa anaweza kuhitaji vifaa maalum ili kutembea, au asiweze kutembea kabisa na aweze kuhitaji msaada wa maisha kwa muda wote.
Na mtu mwenye utindio wa ubongo kwa kiasi kidogo anaweza kutembea kwa taabu kidogo lakini asiweze kuhitaji msaada wowote.
Watu/watoto wote wenye utindio wa ubongo hupata matatizo ya mwendo na mkao….. Wengi pia huwa na hali nyingine zinazoambatana na utindio wa ubongo kama vile ulemavu wa akili, kifafa (degedege), matatizo ya kuona, kusikia au kuzungumza, mabadiliko katika uti wa mgongo na matatizo ya viungo kukakamaa kwa misuli au viungo.
Je, Nini husababisha Utindio wa Ubongo?
Utindio wa Ubongo husababishwa na ukuaji usio wa kawaida wa ubongo au kuumia kwa ubongo unaoendelea kukua, jambo linaloathiri uwezo wa mtoto kudhibiti misuli yake.
Awali, watu walidhani kwamba utindio wa ubongo husababishwa hasa na upungufu wa oksijeni wakati wa kujifungua, lakini sasa wanasayansi wanaamini kuwa hali hiyo inachangia asilimia ndogo tu ya visa vya utindio wa ubongo.
Hivyo maendeleo yasiyo ya kawaida au majeraha ya ubongo yanatokea kabla ya kuzaliwa, wakati wa kuzaliwa, ndani ya mwezi mmoja baada ya kuzaliwa, katika miaka ya awali ya maisha ya mtoto na wakati ubongo bado unaendelea kukua, hizi zote zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni:
Moja, Utindio wa ubongo wa kuzaliwa ambao ni aina ya utindio wa ubongo inayotokea kutokana na matatizo ya ubongo kabla ya kuzaliwa au wakati wa kuzaliwa ikiwa asilimia kubwa ya utindio wa ubongo (takriban 85% hadi 90%) ni ya kuzaliwa.
Mara nyingi, sababu halisi ya kutokea kwa hali hii haijulikani.
Lakini pili ni Utindio wa ubongo wa baada ya kuzaliwa….ambapo Idadi ndogo ya visa vya utindio wa ubongo husababishwa na matatizo ya ubongo yanayotokea zaidi ya siku 28 baada ya kuzaliwa.
Utindio wa ubongo wa aina hii huambatana mara nyingi na maambukizi ya ubongo pamoja na majeraha ya kichwa.
Kwa ujumla visababishi vikuu vya utindio wa ubongo ni kukosa hewa (oksijeni) wakati wa kuzaliwa, kuzaliwa kabla ya muda (njiti), manjano kali kwa mtoto mchanga, majeraha ya kichwa katika miaka ya awali pamoja na homa ya uti wa mgongo au degedege.
Dalili za Utindio wa Ubongo kwa Watoto ni zipi….
Wataalam wanasema dalili zake hutofautiana sana kwa sababu kuna aina nyingi na viwango tofauti vya ulemavu huku Ishara kuu kwamba mtoto huenda ana utindio wa ubongo ni kuchelewa kufikia hatua muhimu za ukuaji (kama vile kujigeuza, kukaa, kusimama, au kutembea).
Ni muhimu kutambua kwamba watoto wengine wasiokuwa na utindio wa ubongo pia wanaweza kuwa na baadhi ya dalili hizi hivyo ni vema kuwaona wataalamu wa afya au kumpeleka mtoto hospitalini pindi uonapo dalili hizi.
Na sasa tuangalie, Matibabu ya Utindio wa Ubongo
Wataalam wanasema Hakuna tiba kamili ya utindio wa ubongo, lakini utambuzi wa mapema na matibabu ya haraka vinaweza kuboresha maisha ya watu wenye hali hii hivyo ni muhimu kuanza mpango wa matibabu haraka iwezekanavyo.
Baada ya mtoto kugundulika kuwa ana utindio wa ubongo, kikundi cha wataalamu wa afya hufanya kazi kwa pamoja na mtoto na familia yake ili kuandaa mpango wa kumsaidia mtoto kufikia uwezo wake kamili.
Lakini msaada wa familia na mapenzi ya dhati huongeza matumaini kwa mtoto mwenye utindio wa ubongo
Na kabla ya kuchagua mpango wa matibabu, ni muhimu kuzungumza na daktari wa mtoto ili kuelewa kikamilifu faida na hatari zinazoweza kutokea.
Pia ni muhimu jamii kutambua kuwa utindio wa ubongo si ugonjwa wa kuambukiza, na watoto wenye hali hii wanaweza kufikia mafanikio makubwa endapo watapatiwa msaada sahihi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: