DKT. MWIGULU AAGIZA MKANDARASI WA BWAWA BONDE LA ZIWA EYASI ASAKWE, AKAMATWE
Автор: KINDAI PLUS
Загружено: 2026-03-06
Просмотров: 222
Описание:
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kuzuiwa kwa Hati ya Kusafiria ya mkandarasi wa kampuni ya (Tunnel Sadd Ariana Company) Ariana Co, baada ya kushindwa kutekeleza ujenzi wa Bwawa la Eyasi lililopo Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha.
Dkt. Mwigulu amesema mkandarasi huyo tayari alipokea malipo ya awali ya shilingi bilioni 3 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, lakini alishindwa kufanya hivyo.
Amesisitiza kuwa Serikali haitamvumilia mkandarasi yeyote anayeshindwa kutekeleza wajibu wake baada ya kupokea fedha za umma, na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa ili kulinda rasilimali za Serikali na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati.
Kindai Plus ni television ya mtandaoni inayotoa maudhui ya habari,michezo,burudani,siasa na matukio ya kijamii yanayojili duniani
USISAHAU KUSUBSCRIBE CHANNEL YETU.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: