UTABIRI WA TMA HAUHALALISHI BEI ZA BIDHAA KUPANDISHWA - WAZIRI MKUU
Автор: Daily News Digital
Загружено: 2026-01-29
Просмотров: 13
Описание:
DODOMA: WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara nchini kutowaumiza Watanzania kwa kupandisha bei za bidhaa hususani kipindi hiki cha kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na mfungo wa Kwaresma kwa kuwa nchi kwa sasa haina upungufu wa chakula.
Amesema licha ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) nchini kutangaza kuwepo kwa upungufu wa mvua katika maeneo mengi nchini lakini nchi ina utoshelevu wa chakula hivyo hakuna sababu ya kupandisha bei za vyakula.
Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi, Januari 29, wakati akijibu swali la Nancy Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum katika kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali imejipangaje kuhakikisha nchi inakuwa na utoshelevu wa chakula na kuzuia mfumuko wa bei kuelekea kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Kwaresma.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: / spotileo-176. .
HabariLeo: / habarileo
DailyNews: / dailynewstz
INSTAGRAM;
HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig...
SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid...
TWITTER;
Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: