KIONGOZI WA JUMUIYA BABATI AJINYONGA BAADA YA KUREJEA SAFARI YA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA MOSHI
Автор: Revivalfmtz
Загружено: 2026-01-03
Просмотров: 4220
Описание:
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Maria Justin Tarimo maarufu kama “Mama Mchaga” (43), mjasiriamali na mkazi wa Kitongoji cha Sau, Kijiji cha Matufa, Kata ya Magugu, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, amekutwa amefariki dunia asubuhi ya leo Januari 3, 2026, ndani ya chumba chake kwa kujinyonga kwa kutumia kamba ya Manila.
Akithibitisha tukio hilo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Sau, Amandi Simon, amesema marehemu alikutwa ndani ya chumba chake ambacho pia kilikuwa kikitumika kama duka.
Kwa mujibu wa Elizabeth Kostantino, jirani wa karibu wa familia hiyo, amesema aliitwa na mume wa marehemu baada ya kurejea nyumbani akitokea eneo lao la biashara ya mgahawa, alikokuwa amepeleka vifaa vya kazi kwa kutumia pikipiki.
Mwenyekiti wa Kitongoji amesema Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya uchunguzi na taratibu za kisheria, ambapo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Kituo cha Afya Magugu.
Imeelezwa kuwa marehemu alirejea nyumbani tarehe 2 Januari, 2026 majira ya saa tisa alasiri akitokea mkoani Kilimanjaro, alikokuwa ameenda kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka pamoja na familia yake.
Marehemu alikuwa akijishughulisha na shughuli za mama ntilie katika eneo la Matufa, huku mume wake akiwa dereva wa bodaboda katika kijiwe cha Matufa, na pia akihudumu kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Fransisko Kigango cha Matufa, Parokia ya Magugu.
Mume wa marehemu, alipoombwa kuzungumzia tukio hilo, alishindwa kufanya hivyo kutokana na mshtuko alioupata, na kuomba kupewa nafasi ya faragha.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: