#KURUDI_KWENYE_ASILI_YANGU
Автор: ROHO M TV 111
Загружено: 2024-06-12
Просмотров: 25
Описание:
UMUHIMU WA KUTEMBEA NA KIBALI CHA MUNGU
UTANGULIZI
Kibali kinamahusianoa makubwa sana na maisha ya mwanadamu. Bila kibali unaweza usifike kwenye hatima yako, waliofanikiwa na wakati wengine kuwashinda adui zao walikuwa na kibali.
Kuishi maisha nje ya asili ya Mungu, ni sawa na kuishishi jangwani, kwani utakimbiwa na watu na kila ufanyacho akitakuwa na wafuasi.
Kaini aliomba angalau awe na kibali kwa watu ili wasije wakamua.
Mwanzo 39:21-23
KIBALI CHA YUSUFU
i. Kilimfanya akubalike kwa mkuu wa gereza
ii. Kilimfanya awasimamie wengine (kuwa kiongozi wa wafungwa) na kuishi nje ya mateso ya gerezani
Mungu aliyafanikisha yote aliyoyafanya.
Mungu anajaribu kutuonyesha umuhimu wa kibali na ukiwa nacho kitakupa;
Fedha
Wasaidizi wa hatima yako
Kupendwa kila maeneo
Kibali ni nini?
MAANA YA KIBALI
i. Kukubalika mbele za Mungu
(“Na yule mtoto, Samweli, akazidi kukua akapata kibali kwa BWANA, na kwa watu pia.”) 1 Sam 2:26
ii. Ni kupewa nafasi kwenye moyo wa mtu au mioyo ya watu.
(2 Wakorintho 7:2, “Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu.”)
Kibali ni kitu cha kiroho kwanza kabla hakijaonekana kwa jinsi ya mwili.
Kibali halisi lazima kitoke kwa Mungu mwenyewe na kisichotoka kwa Mungu hakidumu.
Kuna nguvu na maisha zaidi pale unapopata kibali kwa Mungu kwanza, ndipo akupe kibali machoni pa watu.
Kinachotangulia kabla ya kibali ni Neema. Tuangalie kwenye neno hili,
Neema hutangulia ndipo kibali hufuatilia. Unapoona una karama ya uimbaji tambua Mungu alikupa Neema kisha akaachia karama ndani, hivyo karama na Neema hufanya kazi Pamoja. Unapoona unafanya jambo fulani na linaenda vizuri ujue Neema ya Mungu ilitangulia.
JINSI YA KUPATA KIBALI
Kibali cha Mungu kinapatika kwa kutenda vema
“BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde. Mwa 4:6-7
M
Mwanzo 37:3-5.
kibali kina vita ndani yake.
Kabla ya kufanya jambo tafuta kibali cha Bwana kwanza. Samweli alipata kibali machoni mwa Bwana na watu kabla ya kuanza huduma yake.
Kibali cha Bwana kina gharama yake na kinatunzwa. Kinahitaji matunzo na ili utambue au kutunza kibali inatakiwa kuitunza Neema iliyokupa kibali
Waebrania 12:15,
Gharama ya kutunza kibali.
utakatifu.
Uaminifu
Unyenyekevu
Maombi
Danieli 6:4,
Kibali huja na majukumu. Mungu hawezi kukupa kibali bure anakupa na kazi ya kufanya. Usipotimiza jukumu lake atakiondoa kibali.
KIBALI CHA ESTA
Mungu alimpa kibali chake kilichompa kibali mbele za watu waliomwona na mbele za mfalme.
Esta 2:15.
Kibali cha Esta kilikua na kazi ya kufanya hakikuja bure.
Jukumu alilipewa Esta ni kupangua waraka wa hamani na kuwakomboa wayaudi na mauti.
Wakati wa kibali cha Esta kutimiza jukumu lake vita ya kibali iliinuka.
Esta 4:11.
Vita ya kibali haiinuki wakati wowote, huinuka wakati wa kuanza kutimiza jukumu.
Kibali cha Esta kiliachilia hekima na mbinu ya kutekeleza mbinu za kibali.
KIBALI CHA YUSUFU
Mungu alimpa Yusufu kibali na akapata kibali mbele ya baba yake kuliko watoto wengine wote.
Alipata kibali kwa kila aliyekua anamuona.
Mwanzo 37:3.
Kibali cha Yusufu kilikua na kazi, kilikua kimebeba haya yafuatayo.
Kibali cha Yusufu kilikua kimebeba baraka ndani yake.
Mwanzo 39:5
– Kibali cha Yusufu kilikua kimebeba uongozi
– Kibali cha Yusufu kilikua kimebeba kumcha Bwana
Mwanzo 39:9.
– Kibali cha Yusuph kilikua kimebeba hekima ya kufasiri ndoto
Mwanzo 40:9-19.
– Kibali cha Yusuph kilikua kimebeba maisha ya watu wengi ikiwepo ndugu zake kipindi cha njaa.
Mwanzo 45:5-6
– Kibali cha Yusuph kilikua kimebeba elimu ya wakati ujao (jicho linaloona kesho)
Gharama ya kibali cha Yusufu kilikua ni utakatifu yaan kujitunza nafsi.
Mwanzo 39:9.
9. Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
Matendo ya Mitume 20:28.
28. Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
Kibali cha Yusufu kilipata shambulio.
Shambulio la kwanza la kibali cha Yusufu kilikua kwenye familia yake.
Mke wa Potifa alimpiga vita Yusufu
Mwanzo 39:6.,7.,8.,9.,10.,11.,12.,13.,14.,15.,16.,17.,18.,19.,20.,21.
Wakati unapigwa vita juu ya kibali chako Mungu humwinua mtu kwa ajili yako. Kuna shambulizi la kibali linaumiza lakini ndilo linalokupeleka kwenye hatma yako.
Kuna wakati unatakiwa kukushambuliwa ili wakupeleke kwenye hatma yako. Shambulizi la ndugu wa Yusufu lilipelekea Yusufu kufikia kwenye hatma yake. Shambulizi la kibali lilimpeleka Yusufu gerezani.
Pastor Dr. SWEYA EMMANUEL PAUL
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: