SERIKALI YATOA BILIONI 6.8 MIKOPO YA ASILIMIA 10 MKOANI TANGA
Автор: TANGA MKOA TV
Загружено: 2026-01-05
Просмотров: 142
Описание:
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, amesema kuwa Mkoa wa Tanga umefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025, tangu ruhusa ilipotolewa kwa Halmashauri kuanza kutoa mikopo ya asilimia 10.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo hiyo mkoani Tanga, Prof. Shemdoe amesema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 3.8 zimetokana na makusanyo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, huku shilingi bilioni 3.4 zikitokana na marejesho ya mikopo iliyotolewa awali, jambo linaloonesha umuhimu wa urejeshaji wa mikopo kwa wakati.
Amesisitiza kuwa mikopo hiyo inaposisitizwa irejeshwe, lengo lake ni kuwawezesha wanufaika waliopo na vikundi vipya kupata fursa ya kukopa, akieleza kuwa urejeshaji mzuri wa mikopo utawezesha serikali kuongeza kiwango cha fedha kitakachotolewa katika miaka ijayo.
Katika hafla hiyo, serikali imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 2.761 kupitia Halmashauri za Jiji la Tanga, Lushoto, Korogwe na Pangani, fedha ambazo zimevikutanisha vikundi 155 vya wanawake, 71 vya vijana na 19 vya watu wenye ulemavu, na kutengeneza jumla ya ajira 1,715.
Prof. Shemdoe amesema utoaji wa mikopo hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100 za kuimarisha uchumi wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya asilimia 10.
Ameelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Masuhuli kuhakikisha mikopo yote inayotolewa inarejeshwa kwa wakati, huku Maafisa Maendeleo ya Jamii wakitakiwa kuhakikisha mikopo hiyo inawafikia wananchi katika kila kata, kwa kuwasaidia wenye uhitaji kujaza fomu za mikopo bila vikwazo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, amesema kuwa tangu kuteuliwa kwa Mheshimiwa Rais, mkoa huo umeanza kutekeleza ahadi zake kwa vitendo, ambapo ndani ya kipindi cha chini ya miezi sita tayari shilingi bilioni 2.6 zimetolewa, na ifikapo mwisho wa mwaka kiasi cha mikopo kinatarajiwa kufikia takribani shilingi bilioni 8.
Nao wanufaika wa mikopo hiyo kutoka vikundi mbalimbali wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, wakisema mikopo hiyo imewawezesha kuanzisha na kupanua shughuli za kiuchumi, kuongeza kipato na kutoa ajira kwa vijana wengi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: