GSM KAMPUNI YA KWANZA KULETA GARI ZA HOWO MAX 400
Автор: Media Wire
Загружено: 2025-11-28
Просмотров: 467
Описание:
Kampuni ya GSM Group imeandika historia mpya baada ya kupokea magari 100 ya kubeba mafuta (petroleum tankers) aina ya HOWO Max 400, ikiwa ni awamu ya kwanza ya mpango wao wa kuongeza uwezo wa usafirishaji nchini.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya magari hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa GSM, Benson Mahenya, alisema kampuni hiyo inatarajia kupokea awamu ya pili ya magari 100 ndani ya siku 21 zijazo. Hatua hiyo inalenga kutimiza lengo la kuwa na magari 200 ya mafuta kabla ya mwaka 2025 kuhitimishwa.
Mahenya alibainisha kuwa GSM ndiyo kampuni ya kwanza nchini kuingiza magari ya aina ya HOWO Max 400 yaliyotengenezwa maalum kwa ajili ya kubeba mafuta, hatua inayoongeza chachu kwenye ukuaji wa sekta ya usafirishaji Tanzania.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: