TABORA YA VIWANDA YAJA, EKARI 150 WATENGEWA WAWEKEZAJI
Автор: Daily News Digital
Загружено: 2026-03-07
Просмотров: 4
Описание:
NA Michael Samwel-Tabora
Zaidi ya Watanzania laki tano wanaoishi Mkoa wa Tabora wanatarajiwa kunufaika na ajira rasmi na zisizo rasmi kufuatia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2025 ambapo Kupitia mpango huo eneo maalum la ekari 150 limetengwa katika kata ya Kalunde, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, kwa ajili ya kuanzisha kongani ya viwanda itakayohamasisha sekta binafsi kuwekeza katika viwanda vitakavyotumia malighafi za ndani na nje ya nchi, hatua itakayosaidia kuongeza thamani ya mazao na malighafi zinazozalishwa ndani ya halmashauri.
Taarifa hiyo imetolewa wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2025 katika Manispaa ya Tabora, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Upendo Wella, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Halmashauri Kuu ya CCM wilaya, amesema kuwa zaidi ya Sh bilioni 1.6 zimetolewa kwa vikundi mbalimbali vya wananchi. Aidha ameeleza mafanikio mengine ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo mashuleni, uboreshaji wa barabara pamoja na sekta za kilimo, mifugo na afya, huku akisisitiza kuwepo kwa fursa nyingi za uwekezaji kwa Watanzania waliopo ndani na nje ya mkoa wa Tabora.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: