ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

Salama Na MR BLUE SE6 EP69 KHERI PART 1 SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Автор: YahStoneTown

Загружено: 2023-05-29

Просмотров: 187044

Описание: #SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460

Kheri Sameer aka Mr Blue aka Lil Sama aka Bayser ni mdogo wangu, mdogo wangu kabisa na uzuri nakumbuka kabisa mara ya kwanza kuonana nae na mpaka alivyokua amevaa. Jezi ya Denver Nuggets, jeans ya light blue na sneakers nyeupeeehh na chain ya Silver, kwenye maskio alikua na hereni za kung’ara zile ambazo zilikua si za kitoboa skio, zilikua zina smaku na nazijua zaidi kwasababu Marehemu cousin brother wangu alikua nazo maana nyumbani ilikua hairuhusiwi kutoboa maskio enzi hizo. Alikua msafi, ana swagg ya kuongea na hata jinsi alivyokua anajibeba. Alikua wa moto sana unaweza kusema hivyo, au niseme hivyo. Kila ‘mtoto’ na kijana alitamani kuwa kama yeye kwa kila kitu, muonekano mpaka hit songs kwenye radio na TV.

Blue alikua na mtu ambaye anamsimamia na huyo hakua mwengine bali G Lover, meneja na Dj ambaye alikua anasimamia kazi zake yeye pamoja na wasanii wengine kama Ally Kiba, Ally Com na Abby Skills kwa kuwataja kwa uchache na wasanii wake hao wote walikua wa moooto sana. Ngoma kali, video mbaya, show nyingi na kwa ‘mhindi’ wanauza sana. Na kuanzia hapo kwa mhindi na kuuza sana ndo ambapo kuliweza kuwapoteza wengi kwasababu wengi walikua wadogo sana na pesa ilikua nyingi. Fitna na utovu wa nidhamu wa kupindukia ulianzia hapo. Wakati naandika hii nilimuwaza Ally Kiba na jinsi ambavyo ameweza ku maintain class flani toka siku ya kwanza tunamskia na mpaka leo regardless ya mengi ambayo yametokea hapo katikati, HAKUWAHI KUPOTEA. Kwa hilo naamini anastahili HESHIMA na recognition ya hali ya juu pengine kuliko tunayompa maana dah, mambo yalikua mengi sana enzi hizo.

Kuna usemi kwamba wakati ni mwalimu mzuri sana na kwa uelewa wangu hakuna ambaye anaweza kuelezea experience kama ilivyo elezewa kwenye usemi huo. Wakati ndo ambao unatufunza na kutuonyesha vitu na watu wengi, ambao tulikua tukiwaamini na wengine kuto kuwaamini, kuwapenda na wengine kuto wapenda, kudhani unajua na ki ukweli hujui, kudhania umezama kwenye dimbwi na mapenzi na huyo alo nae ndo wako wa milele na kumbe si hivyo na hayo yote unayaelewa within kipindi fulani, miaka inavyokwenda ndo na wewe unaelewa na kujifunza mambo kwa uwezo na uelewa wako. Moment za ‘anha’ na ‘wow’ huwa nyingi sana. Wakati ni MWALIMU na majuto huwa ni mjukuu, nadhani utakua umenielewa.

Mr Blue alikua na dunia kwenye miguu yake, ilikua yeye tu aseme anatakaje na anataka ielekee wapi na hivyo ndo ingekua ila haikua hivyo ndo jambo la kusikitisha lakini bahati kubwa ambayo mwenzetu alikua nayo au yuko nayo ni kwamba hayo yote yalitokea mapema sana, wakati yuko mdogo sana kwenye dunia ambayo wengi walikua wakimuangalia na kumpenda sana. Yeye baada ya kuona mapenzi na shangwe hilo basi akadata na akaanza kuwa mgumu kufanya nae kazi, akawa na marafiki tele ambao hakua anawajua kabla hajawa Lil Sama na baadae Mr Blue. Akawa hasikii la muadhini wala mnadi sala. Akajiingiza kwenye uvutaji wa bangi isokua na staha, akaondoka nyumbani na kwenda kuishi kwenye ma ghetto na wana wasokua na ramani. Akawa ana party Jumatatu mpaka Jumatatu. Studio haonekani, kwenye interview hatokei na wale watangazaji ambao walikua wanapiga mgoma zake kwenye Radio akawa hata salaam hawapi. Producer na meneja nao wakagombana nae kwasababu sitofahamu ya pesa kwa mhindi ilishika hatamu.

Mwanzo nilisema Blue ana Kheri sana kama jina lake kwasababu hayo yote yalitokea wakati mdogo sana, dunia ilimfunza nae akafundishika, wakati dunia hiyo ikiwa inamfunza alikua mwanafunzi mzuri sana kwasababu darasa alilolipata wakati kakata ringi ndo ambalo limefanya awe BORA na ajitambue LEO HII.
Kwenye meza yetu ya kigae na kiti chakavu Blue ananielezea hustle zote ambazo alishawahi kuzipitia wakati anakua na huku akiwa anajitafuta na kwa uelewa wangu itasaidia wengi ambao wanaaza au wataanza kuzishika pesa mapema au hata ambao watapata mafanikio huko mbeleni watajua jinsi ya ‘kujibeba’ kutokana na maongezi yetu haya.

Tafadhali enjoy.

Love,
Salama.

Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs

Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬
‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa

Soundtrack Yeah by @MarcoChali    • Marco Chali Feat One The Incredible & Msam...  

Follow:
Twitter:   / yahstonetown  
Instagram:   / yahstonetown  
Facebook:   / yahstonetown  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
Salama Na MR BLUE SE6 EP69 KHERI PART 1 SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

Salama Na FETTY DENSA SE6 EP70 KUTOKA UBAVUNI PART 2 SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na FETTY DENSA SE6 EP70 KUTOKA UBAVUNI PART 2 SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na MR BLUE SE6 EP69 KHERI PART 2 SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na MR BLUE SE6 EP69 KHERI PART 2 SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1

Salama Na Idris Ep 8 | TROOPER Part 1

BSS 2022 SE13EP03 SALAMA JABIR FULL SHOW

BSS 2022 SE13EP03 SALAMA JABIR FULL SHOW

MR BLUE AMKATAA JOH MAKINI LIVE,SIO MWAMBA,SIWEZI KUMDISS,KINYAGO NAKUCHONGA UNANITISHA?

MR BLUE AMKATAA JOH MAKINI LIVE,SIO MWAMBA,SIWEZI KUMDISS,KINYAGO NAKUCHONGA UNANITISHA?

SIMBA ANGURUMA 🦁||AMEZUNGUMZIA YALE YOTE YALIOJIRI KULE FURAHA CITY FESTIVAL. ISSUE KUHUSU WILLYPAUL

SIMBA ANGURUMA 🦁||AMEZUNGUMZIA YALE YOTE YALIOJIRI KULE FURAHA CITY FESTIVAL. ISSUE KUHUSU WILLYPAUL

Salama Na KING AliKiba SE6 Ep 03 FULL SHOW | DELIGHTFUL Part 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460

Salama Na KING AliKiba SE6 Ep 03 FULL SHOW | DELIGHTFUL Part 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460

MR BLUE afunguka kilicho MPONZA mpaka KUFULIA kisa UMAARUFU/KIINGEREZA kilivyo mkosesha KAZI....

MR BLUE afunguka kilicho MPONZA mpaka KUFULIA kisa UMAARUFU/KIINGEREZA kilivyo mkosesha KAZI....

TOBAAH! SALAMBA AVUJISHA SIRI DEPU KUSAINI YANGA! KWA USAJILI HUU YANGA WAMELAMBA DUME SIKIA HAPA..💪

TOBAAH! SALAMBA AVUJISHA SIRI DEPU KUSAINI YANGA! KWA USAJILI HUU YANGA WAMELAMBA DUME SIKIA HAPA..💪

DUUH/ YONA ALIEKUA CHADEMA AFICHU MAZITO YA HECHE NA CHADEMA KUTEKA NA KUUWA WATU/ KUFUNDISHA UASI..

DUUH/ YONA ALIEKUA CHADEMA AFICHU MAZITO YA HECHE NA CHADEMA KUTEKA NA KUUWA WATU/ KUFUNDISHA UASI..

MANARA AMBANANISHA CHID BENZ MASWALI MAGUMU SANA / KWANINI ULIAMUA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

MANARA AMBANANISHA CHID BENZ MASWALI MAGUMU SANA / KWANINI ULIAMUA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA

Safari Ya Adam Mchomvu, Kusoma Uganda Mpaka Kufanya Kazi Clouds | SALAMA NA ADAM MCHOMVU PART 1

Safari Ya Adam Mchomvu, Kusoma Uganda Mpaka Kufanya Kazi Clouds | SALAMA NA ADAM MCHOMVU PART 1

DIAMOND VS ALI KIBA, MR BLUE AWEKWA KATI | JINA LA

DIAMOND VS ALI KIBA, MR BLUE AWEKWA KATI | JINA LA "SIMBA" LILILETA UGOMVI | USELA UMEUA MICHARAZO

JAY MOE asimulia alivyomkutanisha NGWAIR na P-Funk ‘Alikuwa ameajiriwa kwenye kibanda cha simu’ Pt2

JAY MOE asimulia alivyomkutanisha NGWAIR na P-Funk ‘Alikuwa ameajiriwa kwenye kibanda cha simu’ Pt2

Salama Na NANDY Ep 53 | MNOGESHAJI PART 1

Salama Na NANDY Ep 53 | MNOGESHAJI PART 1

IBADA KUBWA YA KUNG'OA MIZIZI YA DHAMBI IKIONGOZWA NA MCHUNGAJI HANANJA

IBADA KUBWA YA KUNG'OA MIZIZI YA DHAMBI IKIONGOZWA NA MCHUNGAJI HANANJA

TAZAMA UJENZI WA DARAJA LA PANGANI ULIPOFIKIA // ZIARA YA BODI YA USHAURI YA TANROADS  DISEMBA 2025

TAZAMA UJENZI WA DARAJA LA PANGANI ULIPOFIKIA // ZIARA YA BODI YA USHAURI YA TANROADS DISEMBA 2025

Otworzyli TAJNY Bunker Stalina Po 75 Latach—To, Czego Ci NIGDY Nie Powiedziano

Otworzyli TAJNY Bunker Stalina Po 75 Latach—To, Czego Ci NIGDY Nie Powiedziano

GSM: MAMA YANGU ALINISIHI SANA NIWE KARIBU NA NDUGU ZANGU, NINAHESHIMU WATU WOTE MASIKINI AU TAJIRI

GSM: MAMA YANGU ALINISIHI SANA NIWE KARIBU NA NDUGU ZANGU, NINAHESHIMU WATU WOTE MASIKINI AU TAJIRI

Maisha Ya Bien – Siri, Changamoto Na Mafanikio Yote | Simulizi Kali Ya Msanii Mkubwa Kenya

Maisha Ya Bien – Siri, Changamoto Na Mafanikio Yote | Simulizi Kali Ya Msanii Mkubwa Kenya

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]