RAIS WA MADAGASCAR AWASILI TANZANIA.
Автор: MFA_Tanzania
Загружено: 2023-07-26
Просмотров: 1901
Описание:
Tanzania inaendelea kuwapokea Viongozi kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wanaokuja nchini kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu rasilimali watu.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, imeshuhudiwa ndege nyingi zikitua ambapo kati ya ndege hizo ilikuwa ni ndege iliyombeba Rais wa Madagascar Mheshimiwa Andry Nirina Rajoelina ambayo ilitua nchini Julai 25, 2023.
Waziri Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mudrick Sarogha pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Madagascar mwenye makazi yake Maputo, Msumbiji Kamishna Jenerali wa Magereza Mhe. Balozi Phaustine Martin Kasike walikuwepo uwanjani hapo kumpokea Mh. Rajoelina
Mkutano huo unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, umeanza Julai 25, 2023 kwa ngazi ya Mawaziri na Julai 26, 2023 utahitimishwa kwa ngazi ya Wakuu wa Nchi na Serikali.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: