ARSENAL HAWATAKI SHIDA| UEFA KAZI IPO PLAY OF NI VIGOGO WOTE WANAKUTANA HUKO
Автор: Talent Media
Загружено: 2026-01-29
Просмотров: 677
Описание:
#caf #azamtv #cafcc #cafcl #talenttv #nguvumoja #reporter #yangasc #simbasc #live
Ligi kuu ya Uingereza imeweka rekodi nzuri msimu huu kwa kuingiza vilabu vitano katika hatua ya 16 bora ya michuano ya UEFA.
Vinara kwenye michuano hii ambao ni Arsenal wamedumisha rekodi yao nzuri kwa ushindi mwingine 3-2 dhidi ya Kairat Almaty. Liverpool, Tottenham, Chelsea na Manchester City wametinga hatua ya nane bora.
Msimamo wa mwisho unaonyesha uimara wa Ligi Kuu ya Uingereza. Timu tano kati ya nane bora ni vilabu vya Uingereza, huku hakuna taifa lingine lenye zaidi ya timu moja. Ujerumani, Uhispania na Ureno zina mwakilishi mmoja, yaani, Bayern Munich, Barcelona na Sporting CP.
Newcastle ndiyo timu pekee ya Uingereza iliyokosa nafasi ya nane bora lakini imeingia hatua ya mtoano ikiwa ni moja ya timu zilizopanda daraja katika hatua za michuano hii ikiwa imemaliza nafasi ya 12, kumaanisha kwamba Newcastle itamenyana na moja kati ya timu mbili ambazo hazijapangwa katika hatua ya 8 bora. Newcastle inaweza kukipiga na Qarabag au Monaco.
Kulingana na FIFA ligi kuu ya Uingereza ni nambari moja kati ya ligi bora zaidi duniani, ikifuatiwa na Seria A ya Italy, namba tatu ni Spain-Laliga, nne ni German-Bundersliga na nambari tano ni ligi kuu ya Ufaransa.
Kwa msimamo huu wa hatua ya makundi ligi ya uingereza imezidi kudhihirisha kwamba wao ni vinara na wababe wa michuano hii.
Katika hatua ya kushangaza zaidi klabu ya Real Madrid imetupwa nje kwenye hatua ya 8 bora na kulazimishwa kuingia hatua ya mtoano baada ya kuchapwa goli 4-2 na Benfica.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: