Mtuhumiwa wa utapeli, ajifanya Waziri Mchengerwa kumtapeli RC Tabora
Автор: Nukta TV
Загружено: 2026-03-17
Просмотров: 157
Описание:
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia mtu mmoja aitwaye Kange Thabiti (45), mkazi wa Kiloleni mjini Tabora, kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya utapeli kupitia mitandao ya simu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paulo Chacha, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa kufuatia taarifa za kuwepo kwa mtu aliyekuwa akijinasibu kuwa kiongozi wa ngazi za juu serikalini na kutumia utambulisho huo kuwashawishi wananchi pamoja na baadhi ya viongozi wa chama na serikali ili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Alieleza kuwa tukio hilo lilibainika baada ya mtuhumiwa huyo kujaribu kumtapeli yeye mwenyewe kupitia mawasiliano ya simu, jambo lililoibua shaka na kusababisha kufanyika kwa uchunguzi wa kina.
Kutokana na hali hiyo, Kamati ya Usalama ya mkoa iliunda kikosi maalum cha upelelezi na intelijensia kilichofanya operesheni ya kumtafuta mtuhumiwa huyo na hatimaye kufanikiwa kumkamata.
Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa, upelelezi wa awali umekamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: